Pata taarifa kuu
UGANDA-EMIRATES-MHUDUMU

Mhudumu wa ndege aliyeanguka katika uwanja wa Kimataifa wa Entebbe afariki dunia

Mhudumu wa Shirika la ndege la Emirates aliyeanguka akiwa kwenye mlango wa kutokea wa dharura siku ya Alhamisi, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe nchini Uganda, amefariki dunia.

Shirika la ndege la Emirates
Shirika la ndege la Emirates Emirates
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Hospitali ya Kisubi, Francis Sekandi, amesema mhudumu huyo wa kike aliwasili katika hospitali hiyo akiwa ameshapoteza maisha baada ya tukio hilo.

Mamlaka ya safari za ndege nchini humo inasema, inachunguza kisa hicho ambacho sio cha kawaida.

Shirika la Emirates lenye makao yake huko Dubai, linasema mhudumu huyo alionekana kufungua mlango huo wa dharura na kuanguka kutoka kwenye ndege hiyo iliyokuwa imetua na kuegeshwa.

Gazeti la kila siku nchini Uganda Daily Moniter, limeripoti kuwa walioshuhudia wanasema kuwa mhudumu huyo ni kama alianguka kwa makusudi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.