ICC yaruhusu kufanyika kwa uchunguzi kuhusu uhalifu uliofanywa Burundi
Majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya ICC wameidhinisha rasmi kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma za kutekelezwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu nchini Burundi, ambako zaidi ya watu elfu 1 na 200 wamekufa tangu kulipozuka machafuko mwaka 2015.
Imechapishwa:
Kwa mujibu wa maofisa wa mahakama hiyo, wamesema kuwa uamuzi wa majaji ulifanyika mwezi uliopita, siku mbili tu kabla ya Octoba 27 mwaka huu nchi Burundi kuwa taifa la kwanza kujitoa kwenye mahakama hiyo.
Kwenye uamuzi wao, majaji wamemruhusu mwendesha mashtaka mkuu Fatou Bensouda kuanzisha uchunguzi kuhusu makosa yaliyofanyika nchini Burundi au kufanywa na raia wake wanaoishi nje ya nchi kuanzia April 26 mwaka 2015 hadi Octoba 26 mwaka 2017.
Fatou Bensouda anaweza kupanua wigo wa uchunguzi wake kwa makosa yaliyotekelezwa kabla na baada ya tarehe hizo ikiwa misingi kadhaa ya kisheria itafikiwa.
Tayari msemaji wa rais Pierre Nkurunziza Willy Nyamitwe kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter amekashifu uamuzi huu wa majaji aliosema ni sawa na kujipiga risasi mguuni.
La #CPI, corrompue, vient de se tirer encore une balle dans le pied. La tricherie saute aux yeux. Sans doute que le #Burundi sortira vainqueur de cette bataille, c’est la dernière carte de l’Occident. https://t.co/OP3758j4ZQ
Amb. Willy Nyamitwe (@willynyamitwe) 9 novembre 2017
Mahakama hiyo inasema licha ya kuwa Burundi imejitoa rasmi Octoba 27, majaji wamesisitiza kuwa wanayomamlaka ya kuafanya uchunguzi kuanzia tarehe zilizotajwa.