Pata taarifa kuu
BURUNDI-FOCODE-ICC-HAKI

FOCODE yaiomba ICC kuanzisha uchunguzi nchini Burundi

Shirika moja linalotetea haki za binadamu nchini Burundi la FOCODE limeitoa wito kwa mahakama ya kimataifa ya ICC kuanzisha uchunguzi kuhusu makosa yaliyofanyika Burundi tangu mwanzo wa mgogoro wa nchi hiyo mwaka 2015, huku likitoa orodha ya watu waliotoweka katika mazingira ya tatanishi.

Maandamano mjini Bujumbura tarehe 28 Januari 2017 dhidi ya Bunge la Ulaya.
Maandamano mjini Bujumbura tarehe 28 Januari 2017 dhidi ya Bunge la Ulaya. STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano wakati dunia ikiadhimnisha siku ya kimataifa ya kupinga vitendo vya watu wanaotoweka katika mazingira tatanishi, shirika la FOCODE limetaka mahakama ya ICC kuanzisha mara moja uchunguzi kuanzia Octoba 27 mwaka huu kuchunguza mauaji yaliofanyika tangu April mwaka 2015.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na shirika hilo, limeitaka ICC kuwafikisha mahakamani wahusika wote wa mauaji bila kujali nyadhifa zao, huku likitaja pia matukio kadhaa ya watu waliotoweka katika mazingira tatanishi.

Kwa mujibu wa shirikisho la kimataifa la haki za binadamu pamoja na shirika la haki za binadamu la Burundi Lighe Iteka, watu wanaokadiriwa kufikia 800 na 1.200 wametoweka katika mazingira yenye utata tangu kuzuka kwa machafuko kupinga hatua ya raia Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Hata hivyo nchi ya Burundi ni miongoni mwa mataifa yaliyoandika barau ya kujitoa kwenye mkataba wa Roma unaotambua mahakama ya ICC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.