Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI-UHURU KENYATTA-IEBC

IEBC yaahirisha uchaguzi wa marudio Magharibi mwa Kenya

Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imetangaza kuahirisha zoezi la upigaji kura katika kaunti nne ambazo siku ya Alhamisi wananchi wake hawakupiga kura kwa sababu za kiusalama.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya IEBC imekuja saa chache baada ya viongozi wa dini na wanasiasa kwenye kaunti ya Kisumu kuitaka tume hiyo kuondoa masanduku ya kura iliyokuwa imepeleka kwaajili ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika jumamosi.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema kwa sasa uchaguzi huo utapangiwa tarehe nyingine ambayo itatangazwa na tume yake ili kutoa nafasi kwa raia kupiga kura.

“Inapokuja kwa wafanyakazi wetu, pale wanapokuwa hatarini..kama tume tunaguswa sana na kwasababu hiyo, tume imejadiliana kutokana na matukio mbalimbali yanayotokea kwenye sehemu za nchi, imeahirisha uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika Jumamosi hadi katika tarehe nyingine itakayotangazwa”

Katika hatua nyingine kinara wa upinzani Raila Odinga jana jioni alitembelea eneo la Kibera na kuzungumza na wafuasi wake ambao toka siku ya Alhamisi wamekuwa wakikabiliana na polisi ambapo amewataka wasubiri mpaka siku ya Jumatatu ya wiki ijayo ambayo atatangaza uelekeo mpya.

Ziara yake kwenye eneo hili imekuja siku moja baada ya kundi la vijana kuvamia kituo cha mafunzo ya elimu cha Raila mjini Kibera na kuiba vifaa mbalimbali vya kufundishia pamoja na kuchoma moto vitabu vya shule.

Kutokana na uharibifu huu Raila Odinga alitoa ahadi ya juma moja kufanya ukarabati katika shule hiyo.

Katika hatua nyingine matokeo ya kura katika uchaguzi uliofanyika siku ya alhamisi yameendelea kujumuishwa katika ukumbi wa Bomas Of Kenya huku rais Uhuru Kenyatta akiendelea kuongoza dhidi ya wapinzani wengine walioshiriki kwenye uchaguzi.

Wakati huohuo kumeendelea kushuhudiwa vurugu kwenye eneo la Kawangware jijini Nairobi kati ya makundi hasimu mawili ambayo yanadaiwa kuvamia makazi ya watu na kupora mali hali iliyowafanya polisi kuingilia kati.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.