Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Viongozi wa siasa na dini Magharibi mwa Kenya wamesema hawataki Uchaguzi

Wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea nchini Kenya viongozi wa dini pamoja na wanasiasa kutoka eneo la Nyanza kutoka Kaunti za Kisumu, Siaya, Migori na Homabay, wamejitokeza na kupinga uchaguzi uliopangwa kufanyika kesho jumamosi kufuatia kushindwa kufanyika kwa uchaguzi huo wa marudio mnamo tarehe 26 oktoba.

Maandamano mjini Kisumu Oktoba 25 2017
Maandamano mjini Kisumu Oktoba 25 2017 REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati viongozi wa dini na viongozi wa kisiasa, wamesema kuwa uchaguzi uliopangwa kufanyika katika katika nne zilizopo katka eneo la Nyanza zinaweza kusababisha machafuko zaidi.

Aidha viogozi hao wa dini wametoa wito wa kuondolewa kwa maafisa wote wa usalama katika Kaunti hizo na kumtaka Mwenyekiti wa Tume Huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Wafula Chebukati kuyarudisha Nairobi vifaa vyote vya kupigia kura.

'Wasitulazimishe kufanya Uchaguzi, watu wa eneo hili wamesema hawataki kushiriki, tunaomboleza wiki moja,” alisema Profesa Anyang Nyong'o Gavana wa Jimbo la Kisumu.

Watu watatu wamepoteza maisha katika mji wa Kisumu katika makabiliano na Polisi, huku makabiliano yakishuhudiwa siku ya Ijumaa katika Kaunti ya Migoro.

Wapiga kura katika eneo hilo wamesisitiza kuwa hawatapiga kura, wala kujitokeza kushiriki katika zoezi hilo ambalo kiongozi wao amesema wasusie.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.