Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI

Rais Uhuru Kenyatta aongoza kwa kura

Kenya imeendelea kuonekana Ijumaa hii katika hali ya mgawanyiko zaidi kuliko katika kipindi cha wiki za hivi karibuni, siku moja baada ya uchaguzi wa urais wa marudio uliosusiwa na upinzani.

Kadi ya uchaguzi wa urais wa marudio wa Oktoba 26, ambapo idadi ya wapiga kura ilikua ndogo na kushuhudiwa kwa makabiliano kati ya waandamanaji wa upinzani na polisi.
Kadi ya uchaguzi wa urais wa marudio wa Oktoba 26, ambapo idadi ya wapiga kura ilikua ndogo na kushuhudiwa kwa makabiliano kati ya waandamanaji wa upinzani na polisi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa siku ya alhamisi uligubikwa na machafuko yaliyosababisha watu wanne kutoka upande wa upinzani kupoteza maisha.

Machafuko haya katika baaadhi ya maeneo ya nchi hiyo yalisababisha uchaguzi unaahirishwa magharibi mwa Kenya na tayari inasemekana kuwa uchaguzi huo uligubikwa na kasoro nyingi na hivyo kuonekana kuwahaukua wa haki.

Shughuli za kuhesabu kura zilizoanza siku ya Alhamisi usiku, zinaendelea Ijumaa hii. Lakini kulingana na kura ambazo zimehisabiwa, Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta, kutoka jamii ya watu wengi ya Kikuyu, anaongoza kwa asilimia 98 za kura, mpinzaniwake wa kihistoria, Raila Odinga, ambaye aliamua kutoshiriki uchaguzi huo amesem akuwa ucahguzi uliofanyika siku ya Alhamisi Oktoba 26 " unafananishwa na uchaguzi lakini sio uchaguzi" .

Kenya ambayo ni nchi ya wafanyabiashara wengi na ya kwanza kwa uchumi katika Afrika Mashariki, imetumbukia katika mgogoro mbaya wa kisiasa kwa miaka 10, tangu mahakam kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 8, tukio la kwanza barani Afrika. Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi katika uchaguzi huo wa awali dhidi ya Raila Odinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.