Pata taarifa kuu
TANZANIA-AJALI

Watu 12 wauawa baada ya kudumbukia Ziwa Victoria

Watu 12 walipoteza maisha nchini Tanzania siku ya Jumatatu baada ya basi ndogo walilokuwa wanasafiria kudumbukia ndani ya Ziwa Victoria Kaskazini mwa nchi hiyo.

Ziwa Victoria nchini Tanzania
Ziwa Victoria nchini Tanzania Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Rais wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki, John Magufuli, amesema ameshtushwa na kuhuzunishwa mno na vifo hivyo.

Basi hilo lilikuwa linawapeleka abiria katika kivuko cha Feri mjini Mwanza, lilipokosa mwelekeo na kuingia Ziwani.

Vyombo vya Habari nchini humo vinaripoti kuwa watu watatu waliokolewa wakiwa hai.

Ziwa Victoria, mbali na Tanzania, linapatikana pia nchini Uganda na Kenya.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.