Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Rais Uhuru Kenyatta kufungua bunge jipya, upinzani kususia

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atafungua bunge jipya la 12 jijini Nairobi, wakati huu nchi hiyo ikiendelea kujiandaa kushiriki katika uchaguzi mpya wa urais tarehe 17 mwezi Oktoba.

Majengo ya bunge jijini Nairobi
Majengo ya bunge jijini Nairobi www.parliament.go.ke
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, wabunge wa muungano wa upinzani NASA wamesema hawatashiriki katika kikao hicho cha kwanza kinachowakutanisha wabunge na Maseneta.

Upinzani unasema kuwa, hauwezi kwenye kikao hicho kwa sababu haumtambui rais Kenyatta kama kiongozi halali wa nchi hiyo hasa baada ya kufutwa kwa ushindi wake mwezi uliopita.

Kiongozi wa NASA Raila Odinga amewaagiza wabunge wa chama chake katika bunge la kitaifa na lile la Senate kutokwenda katika kikao hicho ambacho amesema ni kikao cha wabunge wa chama cha Jubilee na kiongozi wao.

NASA umeandaa mkutano wa hadhara jijini Nairobi kuwahotubua wafuasi wake na kuwafafanulia ni kwanini umesusia kikao hicho.

Hata hivyo, rais Kenyatta amesema hatajali iwapo wabunge wa upinzani hawatakuja bungeni kuhudhuria kikao hicho muhimu.

Aidha, Kenyatta amesema kuwa iwapo Odinga atashinda Uchaguzi wa mwezi ujao, atatumia wingi wa Maseneta kumwondoa madarakani.

“Hata ikiwa atachaguliwa, tunaweza kumwondoa kupitia bunge ndani ya miezi miwili au mitatu kwa sababu tupo wengi bungeni,” alisema Kenyatta.

Upinzani umelaani matamshi hayo na kusema inaonesha wazi kuwa atashindwa wakati wa uchaguzi wa marudio.

Katiba ya Kenya inaeleza kuwa, ikiwa rais aliye madarakani ataondolewa kwa sababu ya kuvunja katiba ya nchi hiyo, naibu wake atakuwa rais kipindi chote kinachosalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.