Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Odinga aomba mchango wa kampeni, amtaka rais Kenyatta ajiuzulu

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, unadai kuwa baadhi ya Makamishena wa Tume ya Uchaguzi wanatishwa maisha na hata wamepokonywa walinzi wao.

Raila Odinga, kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA
Raila Odinga, kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA Photo: AFP/Kevin Midigo
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga amesema kinachoendelea kinaiweka Tume hiyo katika njia panda ya kusimamia Uchaguzi mpya mwezi Oktoba.

“Tupo katika kipindi kigumu sana, Makamishena wanatishiwa maisha na serikali ya Jubilee,” alisema Odinga.

Aidha, Odinga amesisitiza kuwa alishinda Uchaguzi wa mwezi uliopita na kumtaka rais Uhuru Kenyatta kujiuzulu kwa kile anachosema ameiweka nchi hiyo katika kipindi kigumu cha kisiasa.

“Ningekuwa Uhuru Kenyatta ningeamua kujiuzulu ili kujiepusha na haya yote yanayotokea,” .

Rais Uhuru Kenyatta amekuwa akisema, matamshi anataka kulazimisha kuwepo kwa serikali ya muungano na kuongeza kuwa hataki Uchaguzi huo kufanyika.

Pamoja na hilo, Odinga ameongeza kuwa ujumbe wake uko tayari kukutana na Tume ya Uchaguzi kujadili mambo mbalibali yanayoikabili katika maandalizi yake.

Kumeonekana mgawanyiko ndani ya Tume ya Uchaguzi baada ya Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati kumwandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Ezra Chiloba kutaka atoe majibu ya kilichosababisha mapungufu makubwa wakati wa Uchaguzi uliofutwa.

Hata hivyo, baadhi ya Makamishena wamesema hawafahamu barua hiyo kwa sababu Mwenyekiti hakuwashirikisha.

Pamoja na hayo, Odinga amewaomba wafuasi wake kuchangia fedha kampeni za NASA kuelekea Uchaguzi mpya.

“Tunaomba wafuasi wetu watuchangie chochote walichonacho, ukichangia utakuwa umenunua tiketi yako ya kwenda Canaan,” alisema Odinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.