Pata taarifa kuu
KENYA-KESI-UCHAGUZI

Uamuzi wa kesi ya kupinga ushindi wa rais Kenyatta kufahamika Ijumaa

Majaji wa Mahakama ya Juu wameanza kuandika uamuzi wa kesi ya kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta, iliyowasilishwa na kiongozi wa Muungano wa upinzani NASA Raila Odinga.

Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya
Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya www.kenyaforum.net
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya Majaji hao kutamatisha kibarua cha kusikiliza Mawakili wa upande wa Tume ya uchaguzi, wale wanaomwakilisha rais Kenyatta na wale wa muungano wa upinzani NASA.

Mawakili wa NASA, wakiongozwa na James Orengo, wanataka Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo baada ya kuonesha kuwa kulikuwa na ushahidi mkubwa, Uchaguzi huo haukuwa huru na haki.

Akitoa ripoti ya mwisho, Orengo alisema ikiwa Mahakama hiyo itaangalia kikamilifu ushahidi wote uliowasilishwa, basi ushindi huo utatupiliwa mbali.

Paul Muite anayewakilisha Tume ya Uchaguzi katika kesi hiyo alisema kuwa, pamoja na kwamba huenda kulikuwa na dosaro ndogondogo, zoezi hilo lilikwenda vizuri.

Pande zote mbili, upinzani NASA na Tume ya Uchaguzi iliwasilisha ripoti mbili tofauti zikionesha taarIfa zilizopatikana ndani ya fomu za kujumuisha matokeo lakini pia mitambo ya kuhifadhi matokeo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.