Pata taarifa kuu
KENYA-AJALI

Ajali yasababisha vifo vya watu 11 Pwani ya Kenya

Watu 11 wamepoteza maisha katika ajali ya barabara katika Kaunti ya Tana River Pwani ya Kenya.

Ajali ya basi na Lori nchini Kenya
Ajali ya basi na Lori nchini Kenya PHOTO | COURTESY
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa Polisi katika Kaunti hiyo Walter Aliwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika barabara kuu ya Bangal.

Ripoti zinasema kuwa ajali hiyo ilitokea saa tisa alfajiri wakati basi hilo likielekea  jijini Nairobi, kutoka Wajir.

Abiria nane walikuwa ndani ya basi hilo huku wengine watatu wakiwa ndani ya Lori, lililogongana ana kwa ana na basi hilo la abiria.

Walioponea ajali hiyo wanasema basi hilo liikuwa linaendeshwa kwa mwendo wa kasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.