Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Raila Odinga asubiriwa kutoa kauli baada ya Uchaguzi Mkuu

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, anasubiriwa kutangaza mwelekeo wake kuhusu Uchaguzi Mkuu uliokamilika wiki iliyopita na kumpa ushindi rais Uhuru Kenyatta.

Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, NASA.
Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, NASA. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Odinga aliyewania urais kupitia muungano wa upinzani NASA, na kusema kuwa ndiye aliyeshinda Uchaguzi huo, amekataa kutambua ushindi wa rais Kenyatta na kusema kuwa kura zake ziliibiwa.

Imekuwa ni vigumu kufahamu ni tamko lipi Odinga atasema kwa sababu tayari amesema hatakwenda Mahakamani kupinga ushindi wa rais Kenyatta.

Odinga alitarajiwa kutoa tangazo hilo siku ya Jumanne, lakini baada ya mkutano wa zaidi ya saa sita na vigogo wengine wa upinzani, na kulazimisha tangazo hilo kuahirishwa.

Tume ya Uchaguzi IEBC wakati uo huo bado haijatoa fomu zote za 34 A na 34 B kwa upinzani kama ilivyoombwa, suala ambalo linaendelea kuzua wasiwasi kuhusu uhalali wa Uchaguzi huo.

Tangazo hili linakuja wakati huu, Jumuiya ya Kimataifa ikiendelea kutoa wito kwa Odinga kwenda Mahakamani kupinga ushindi wa Kenyatta.

Kumekuwa na wasiwasi kuwa huenda Odinga akaitisha maandamano yasiyokoma lakini wengine wakisema kuwa huenda akakubali matokeo licha ya kutoridhika nao.

Umoja wa Mataifa umekataa wito wa NASA, kuthathmini namna Uchaguzi huo ulivyofanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.