Raila Odinga : Niko tayari kufichua wizi wa kura
Wakati ambapo hali ya utulivu ikianza kurejea nchini Kenya, kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga akihojiwa na gazeti la Financial Times la Uingereza amesema kwamba atafichua ushahidi siku ya Jumanne kuhusu vile alivyoibiwa kura.
Imechapishwa:
Bwana Odinga amedai kwamba wadukuzi waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na kuweka hesabu ambazo zilimpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta.
“Niko tayari kuonyesha jamii ya kimataifa na Wakenya jinsi gani tulivyoibiwa kura zetu, “ amesema Bwa Odinga .
Raila Odinga ambaye alikuwa akiwania urais kwa mara ya nne alishindwa katika uchaguzi huo wa urais uliyofanyika Agosti 8, 2017. Pia alibaini kwamba hatowania tena urais , huku akisema aliwataka Wakenya kujua kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo.
“Natangazia Wakenya kwamba sitawania tena urais. Tumependelea tu Wakenya kujua mchezo uliopigwa katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017. Sio swala la kuwa mbifansi, Sio swala kuhusu Raila Odinga, “ ameongeza Raila Odinga.
Wakati huo huo Tume ya Uchaguzi imefutilia mbali madai hayo ikibaini kwamba ni madai yasiokuwa na msingi.
Machafuko ya hivi karibuni nchini Kenya yamesababisha vifo kadhaa na watu kadhaa kujeruhiwa na wengine kukamatwa.