Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Rais Kenyatta: Nitakubali matokeo nikishindwa

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema ikiwa atashindwa kwa haki, Uchaguzi Mkuu wa tarehe nane mwezi Agosti, atakubali matokeo na kukabidhi madaraka kwa amani.

Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kenyatta ametoa hakikisho hilo wakati akijibu maswali mbalimbali kupitia runinga na kumtaka mpinzani wake Raila Odinga, naye kuwa tayari kufanya hivyo ikiwa atashindwa katika Uchaguzi huo.

“Mimi ni mtu ninayeheshimu uamuzi wa wananchi, nawaomba wapinzani wangu nao wafanye hivyo. Nawaomba Wakenya kuchukuliana kama ndugu,” alisema rais Kenyatta.

Aidha, amesema serikali yake inalenga kuwa Uchaguzi huu uwe wa amani ndio kwa sababu maafisa wa usalama wamejihami na wako tayari kukabiliana na wale watakaotaka kuzua fujo.

Rais Kenyatta ametoa hakikisho hili siku saba kuelekea siku ya upigaji kura.

Naye Odinga, anayepeperusha bendera ya muungano wa upinzani NASA, naye amekuwa akisema kuwa atakubali matokeo hayo ikiwa Uchaguzi huo utakuwa huru na haki.

Hata hivyo, hivi karibuni ametoa madai mazito kuwa rais Kenyatta anatumia jeshi kumsaidia kuiba kura, madai ambayo serikali imekanusha.

Wapiga kura Milioni 19 wanatarajiwa kupiga kura katika zoezi hili.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.