Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UCHAGUZI

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya kutoingilia matokeo ya majimboni

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imesema haitatangaza matokeo ya urais hatua kwa hatua kama ambavyo imekuwa ikifanyika miaka iliyopita.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati IEBCKenya
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amesema matokeo itakayotoa yatakuwa tu ni yale ya mwisho kutoka majimboni.

Hatua hii imekuja kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu kuwa matokeo ya urais yatakayotangazwa katika majimbo yote 290 ndio yatakayokuwa ya mwisho na hayawezi kubadilishwa na Tume ya Uchaguzi.

Kazi ya Tume sasa itakuwa ni kuyajumuisha na kutoa tangazo la mwisho kwa kuzingatia masharti ya katiba ya nchi hiyo.

Chebukati ameongeza kuwa Tume haitakuwa na uamuzi wa kubadilisha matokeo kutoka majimboni, na kusisitiza kuwa yale yatakayotangazwa ndio yatakayokuwa ya mwisho.

Ikiwa kutakuwa na mgogoro kuhusu matokeo hayo, utaweza kutatuliwa tu Mahakamani.

Mshindi katika Uchaguzi wa urais nchini Kenya, anahitaji kupata angalau asilimia 50 ya kura zote zilizipigwa nchini lakini pia kupata asilimia 25 kutoka kaunti 24 kati ya 47 nchini humo.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wamekuwa wakisema kuwa utaratibu huu utasaidia kuzuia wizi wa kura.

Uchaguzi Mkuu utafanyika tarehe nane mwezi Agosti.

Ushindani mkali wa urais ni kati ya rais wa sasa Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kutoka muungano wa upinzani NASA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.