Pata taarifa kuu
RWANDA-UCHAGUZI

Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda yasema waangalizi 2,000 kushuhudia Uchaguzi Mkuu

Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema waangalizi zaidi ya 1,000 watakuwa nchini humo kushuhudia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 4 mwezi Agosti.

Rais  Paul Kagame akipiga kura katika Uchaguzi uliofika
Rais Paul Kagame akipiga kura katika Uchaguzi uliofika REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Tume hiyo Charles Munyaneza amesema tayari wamepokea maombi ya waangalizi 100, idadi ambayo inatarajiwa kuongezeka zaidi katika siku za hivi karibuni.

Miongoni mwa waangalizi hao ambao wamewasilisha maombi ya kupewa vibali ni mabalozi wa mataifa ya kigeni nchini humo.

Wengine ni kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na waangalizi binafsi nchini humo.

Hata hivyo, Umoja wa Ulaya tayari umesema hautatumia waangalizi wake nchini Rwanda.

Wakati uo huo, msemaji wa Mashirika ya kiraia nchini humo Jean-Léonard Sekanyange, amesema watatuma waangalizi zaidi ya 200 kushuhudia Uchaguzi huo.

Kampeni rasmi za uchaguzi huo, zinatarajiwa kuanza tarehe 14 mwezi Julai na kudumu kwa siku 19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.