Pata taarifa kuu
RWANDA-UCHAGUZI

Kagame aahidi utendaji bora zaidi baada ya kuidhinishwa na RPF kugombea uraisi Rwanda

Raisi wa Rwanda Paul Kagame amekubali hatua ya kuidhinishwa na Chama chake RPF kuwa mgombea wa uraisi kwa mara nyingine katika uchaguzi wa mwezi August mwaka huu.

Raisi wa Rwanda Paul Kagame
Raisi wa Rwanda Paul Kagame REUTERS/Ruben Sprich
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi chama tawala cha RPF nchini Rwanda kilimuidhinisha raisi Paul Kagame kuwa mgombea wake wa uraisi katika uchaguzi wa August.

Hatua hii inakuja baada ya baadhi ya vyama vya upinzani Kutangaza kumuunga mkono raisi Kagame.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa chama hicho raisi Kagame ameahidi kuongeza uwezo wake wa utendaji mara dufu.

Uchaguzi utafanyika mapema mwezi wa nane huku kampeni zikitarajiwa kuanza mwezi ujao Julai.

hatua ya Wabunge nchini Rwanda kupitisha muswada ulioidhinisha kubadilishwa kwa vipengee vya katiba Iliruhusu rais Paul Kagame kuongoza kwa muhula wa tatu.

Takribani Miaka miwili iliyopita Rwanda katika baraza la seneti na bunge ulipitishwa muswada ulioidhinisha kubadilishwa kwa vipengee vya katiba kuruhusu rais Paul Kagame kuongoza kwa muhula wa tatu kama hatua ya mwanzo kuelekea kufanyika mabadiliko ya katiba.

Mamilioni ya raia nchini Rwanda walitia sahihi pendekezo la kumtaka rais Kagame kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kukamilika kwa muhula wake wa pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.