Pata taarifa kuu
KENYA

Watu 26 wapoteza maisha nchini Kenya kutokana na ajali ya barabarani

Watu 26 wamepoteza maisha nchini Kenya na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali katika barabara kuu ya kutoka jijini Nairobi kwenda mjini Mombasa.

Basi lililoharibika baada ya ajali mbaya mjini Kibwezi
Basi lililoharibika baada ya ajali mbaya mjini Kibwezi Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo alfajiri ya leo  na kueleza kuwa basi la abiria liligongana ana kwa ana na trela la mafuta katika mji wa Kibwezi.

“Ilikuwa ni ajali mbaya sana.Tumepoteza watu 26 katika ajali hii,” amesema Leonard Kimaiyo kamanda wa polisi katika mji huo.

Ripoti zaidi zinasema kuwa, basi hilo lilikuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi na kuyapita magari mengine, wakati lilipogongana na trela hilo.

Kenya ni miongoni mwa mataifa ya bara la Afrika yanayoendelea kushuhudia ongezeko la ajali za barabarani mara kwa mara.

Kila mwaka, takwimu zinaeleza kuwa watu 3,000 hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani.

Chanzo kikubwa cha ajali nchini humo ni uendeshaji wa magari kwa mwendo wa kasi, dereva kuendesha gari akiwa mlevi, uchovu wa dereva lakini pia hali mbaya ya barabarani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.