Pata taarifa kuu
TANZANIA-ZAMBIA-UCHUKUZI

Malori 600 ya Tanzania yazuiliwa Zambia, serikali kuingilia kati

Maafusa nchini Tanzania wanasema kuwa wako tayari kuingilia kati ili kutafuta suluhu ya kidiplomasia baada ya Zambia, kuzuia malori 600 ya Tanzania kwa kipindi cha miezi miwili sasa. Hata hivyo maafisa hao hawajasema sababu za kuzuiliwa kwa malori hayo.

Rais wa Zambia Edgar Lungu asema kuwa hatokubali taifa lake kutumika kama kituo cha miti ya mbao akidai kuwa madereva wa malori kutoka Tanzania wanakiuka sheria kuhusu usafirishaji wa mbao.
Rais wa Zambia Edgar Lungu asema kuwa hatokubali taifa lake kutumika kama kituo cha miti ya mbao akidai kuwa madereva wa malori kutoka Tanzania wanakiuka sheria kuhusu usafirishaji wa mbao. M Dawood
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Zambia iliyazuia malori hayo yalipokuwa yakirudi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Inaarifiwa kuwa malori hayo alikuwa yameenda kubeba mbao.

Maafisa wa Tanzania wametoa wito kwa maafisa wao katika ubalozi wao nchini Zambia kuwasilisha swala hilo na maafisa husika ili kupata suluhu ya haraka ili malori hayo yaweze kuachiliwa.

Muungano wa madereva wa malori wa Tanzania Tatao umesema kuwa wanachama wake walifuata maelezo yote kuhusu ununuzi na mauzo ya nje ili kuweza kuingia nchini DR Congo.

Hata hivyo rais wa Zambia Edgar Lungu, siku ya Jumatatu, alisema kuwa hatokubali taifa lake kutumika kama kituo cha miti ya mbao akidai kuwa madereva wa malori kutoka Tanzania wanakiuka sheria kuhusu usafirishaji wa mbao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.