Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Asilimia 60 ya wabunge nchini Kenya hawatachaguliwa tena

Zaidi ya asilimia 60 ya wabunge nchini Kaenya hawatachaguliwa tena wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Ipsos.

Bunge la Kenya
Bunge la Kenya Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Wakenya waliohojiwa wamesema hawatawachagua tena wawakilishi wao wa sasa kwa sababu ya utendajikazi mbaya, hatua yao ya kuhamahama vyama, hali inayoelezwa kuwa ni ya kibinafsi.

Uzoefu wa kisiasa nchini Kenya umeonesha kuwa kwa muda mrefu, wabunge wengi huwa hawachaguliwi tena kurejea bungeni, hali ambayo haitawashangaza wengi.

Utafiti huu umekuja wakati huu Tume ya Uchaguzi ikimaliza zoezi la kuwaandikisha wapiga kura wapya.

Zoezi hilo lilimazika mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya Mahakama kuagiza zoezi hilo kuendelea kwa siku tano zaidi ili kuwapa nafasi wale waliokuwa wamepata vitambulisho vya taifa.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi ambayo ilikuwa imelenga kuwasajili wapiga kura wapya Milioni 6, inasema haitafikia hata nusu ya malengo yao kwa sababu idadi ndogo ya Wakenya walijitokeza kujiandikisha.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati ameahidi kuwa Uchaguzi wa mwezi wa Agosti utakuwa huru, wazi na haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.