Pata taarifa kuu
KENYA

Mahakama ya rufaa nchini Kenya yaagiza kuachiliwa huru kwa viongozi wa chama cha Madaktari

Mahakama ya rufaa nchini Kenya, imeagiza kuachiliwa huru kwa viongozi saba wa chama cha Madaktari waliofungwa jela kwa mwezi mmoja, kwa kukaidi agizo la Mahakama inayoshughulikia maswala ya ajira kusitisha mgomo wa Madaktari unaoendelea.

Mmoja wa Madaktari wakiandamana jijini Nairobi nchini Kenya
Mmoja wa Madaktari wakiandamana jijini Nairobi nchini Kenya Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mawakili wa Madaktari na wale wa wanaowakilisha Baraza la Magavana walikwenda katika Mahakama hiyo baada ya kukubaliana kuwa viongozi hao waachiliwe huru ili mazungumzo yaendelee.

Mahakama imeagiza pande hizo mbili kuanza mazungumzo mara moja na kufikia mkataba wa maelewano kufikia mwisho wa wiki ijayo.

Mazungumzo haya mapya yatawashirikisha pia chama cha Mawakili nchini humo LSK na Tume ya kitaifa ya Haki za Binadamu KNHRC ambayo sasa yataongoza mazungumzo haya.

Maandamano ya Madaktari na wanaharakati nchini Kenya kushinikiza kuachiliwa huru kwa viongozi wa Madaktari
Maandamano ya Madaktari na wanaharakati nchini Kenya kushinikiza kuachiliwa huru kwa viongozi wa Madaktari REUTERS/Thomas Mukoya

Kiongozi wa upinzani nchini huyo na Waziri Mkuu wa zamani aliyekuwa Mahakamani, wakati wa uamuzi huo, ameshutumu serikali kwa kushindwa kutatua mzozo huu.

Aidha, amesema haikubaliki kuwa wakati kama huu rais Kenyatta ameendelea kukaa kimya wakati wagonjwa wakiteseka kutokana na mgomo unaoendelea  kwa zaidi ya siku 70 sasa.

“Hii serikali imeshindwa kutekeleza majukumu yake. Nawaomba Wakenya wenzangu waipelekea  nyumbani tarehe 8 mwezi Agosti wakati wa Uchaguzi Mkuu,” alisisitiza Odinga.

Pamoja na Madaktari nchini humo kutaka nyongeza ya mshahara kwa asilimia 300, inataka pia kuajiriwa kwa Madaktari zaidi, kuboreshewa mazingira ya kufanya kazi lakini pia kununuliwa kwa vifaa vipya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.