Pata taarifa kuu
KENYA-AFYA-MAANDAMANO

Madaktari nchini Kenya waitaka serikali kulegeza msimamo ili warejee kazini

Madaktari wanaogoma nchini Kenya, waiambia Kamati ya afya ya bunge la Senate kuwa wako tayari kulegeza msimamo wao kuhusu madai wanayotaka, ikiwa serikali nayo itakuwa tayari kufanya hivyo.

Mmoja wa madaktari ambao wanashiriki mgomo, wakiandamana hivi karibuni jijini Nairobi.
Mmoja wa madaktari ambao wanashiriki mgomo, wakiandamana hivi karibuni jijini Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa chama cha Madaktari nchini humo Daktari Ouma Oluga amesema kuwa, wanasikitika kuwa baada ya siku sitini ya mgomo hakuna mwafaka wowote uliofikiwa.

Hata hivyo, amesema kuwa wao kama Madakatri wako tayari kulegeza msimamo wao na kurejea kazini ikiwa serikali nayo itafanya hivyo.

Pamoja na Mambo mengine, Madaktari wanataka nyngeza ya mshahara wka asilimia 300 lakini pia kuboreshewa mazingira ya kufanya kazi na kupewa mafunzo zaidi kuhusu kazi yao.

Serikali ya Kenya inasema, haina fedha za kutosha kutekeleza matakwa yao Madaktari hao lakini kwa sasa inaweza kuwaongezea mshahara kwa asilimia 40, nyongeza ambayo madaktari hao wamekataa.

Maseneta wamewasihi Madaktari hao kukubali kurudi kazini, kuwasaidia wagonjwa wanaotafuta huduma katika hospitali za umma.

Mahakama inayoshughulikia maswala ya mizozo ya ajira nchini humo, iimewapa muda madakatri na wadau wnegine kujadiliana kuhusu mgomo huu unaoendelea, la sivyo, iwahukumu kifungo cha mwezi mmoja, viongozi wa Madktatri hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.