Pata taarifa kuu
TANZANIA-USALAMA

Jeshi la polisi Tanzania kukabiliana na watu wanaotoa taarifa za uongo

Jeshi la Polisi nchini Tanzania, limewaonya raia ambao wamekuwa wakipiga simu kwa wapepelezi wa jeshi hilo na kutoa taarifa za uongo kuhusu watuhumiwa wa dawa za kulevya, na kuapa kuwashughulikia raia watakaobainika kutoa taarifa ambazo sio sahihi.

Wakazi wa mji wa Dar es Salaam wamekua wakitoa taarifa kuhusu watu wanaotumia na kufanya biashara ya madawa ya kulevya.
Wakazi wa mji wa Dar es Salaam wamekua wakitoa taarifa kuhusu watu wanaotumia na kufanya biashara ya madawa ya kulevya. Getty Images/Ariadne Van Zandbergen
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro, akizungumza na wanahabari, amesema licha ya kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa zaidi, lakini kumekuwa na wimbi la upotoshwaji wa taarifa.

Kauli yake imekuja ikiwa ni saa chache tu zimepita toka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipotoa orodha mpya ya watuhumiwa wa biashara hiyo, wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara na viongozi wa dini.

Katika hatua nyingine, kamanda Siro, amezungumzia kuhusu kuendelea kuzuiliwa kwa mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu, .

Akizungumza akiwa jijini Dar es Salaam, ni sauti yake, Simon Siro, kamishna wa polisi kanda maalumu ya dar es Salaam, nchini Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.