Serikali ya Tanzania yawataka wapenzi 3 wa jinsia moja kuripoti polisi
Wizara ya Afya nchini Tanzania imewataka watu watatu inaowashutumu kuwa wapenzi wa jinsia moja kuripoti polisi kwa mijali ya kuhojiwa na iwapo hawatofanya hivyo watakamwa.
Imechapishwa:
Naibu waziri wa afya nchini humo Hamis Kingwangalae amebaini kwamba wizara yake inawashtumu watu hao kuambaza harakati za wapenzi wa jinsia moja kupitia mitandao ya kijamii kinyume na sheria.
Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja ni kinyume na sheria nchini Tanzania na watu wanaokabiliwa na hatia hiyo, wanapaswa kupewa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 30 jela.
Serikali imetishia kupiga marufuku makundi ambayo yanaunga mkono haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja.
Itakumbukwa kwamba mwaka uliopita, Waziri wa Afya alitangaza kwamba mpango wa kuwapatia matibabu wapenzi wa jinsia moja walio na virusi vya HIV utasimamishwa.