Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA-USALAMA

Mfalme Mumbere ashtakiwa kwa mauaji wilayani Kasese nchini Uganda

Mfalme wa eneo la Rwenzururu nchini Uganda Charles Mumbere amefunguliwa mashtaka ya mauaji baada ya watu 87 kupoteza maisha mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya makabiliano kati ya maafisa wa usalama na walinzi wake.

Silaha zilizopatikana katika Ufalme wa  Rwenzururu
Silaha zilizopatikana katika Ufalme wa Rwenzururu REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Mumbere alikamatwa akiwa siku ya Jumamosi na kusafirishwa mjini Jinja ambako amekuwa akizuiliwa, lakini amekanusha kuhusika na machafuko hayo.

Serikali ya Uganda inamtuhumu kuwa anaunda kundi la waasi kwa lengo la kutaka kuunda nchi yake itakayoitwa Yiira

Mfalme huyo anatarajiwa kurudi Mahakamani katikati ya mwezi Desemba.

Wachambuzi wa siasa nchini Uganda wanahisi kuwa mgogoro wa Ufalme huu unatokana na ukiukwaji wa haki za binadamu, kutengwa kimaendeleo kwa muda mrefu na suala la uongozi.

Suala la ardhi limekuwa tata sana katika eneo hilo, asilimia 60 ya ardhi katika Wilaya ya Kasese inamilikiwa na serikali na hivyo haiwanufaishi watu wa eneo hilo.

Licha ya Wilaya hiyo kuwa na utajiri wa rasilimali kama Ziwa Katwe, George na Edward. Madini mbalimbali na viwanda kama kile cha Hima, watu wengi katika Wilaya ya Kasese wanaendelea kuishi kwa umasikini na hawana ajira hasa vijana.

Jambo lingine la kutilia maanani ni kuwa eneo la Kasese na Rwenzori lina idadi kubwa ya wapiganaji walioshiriki katika vita dhidi ya Ufalme wa Tooro miaka ya 1960 lakini pia kumsaidia Museveni wakati wa vita vya msituni na sasa hivi wanahisi kuwa hawajalipwa chochote wala kukumbukwa kwa namna yoyote ile.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.