Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-UGANDA

Uganda yafungua kambi mpya kusaidia kuwahifadhi wakimbizi kutoka Sudan Kusini

Kambi ya wakimbizi ya Palorinya nchini Uganda imefunguliwa upya ili kuwapa hifadhi zaidi ya raia 80,000 wa Sudan Kusini wanaokimbia nchi yao kwa sababu ya vita.

Kambi ya wakimbizi ya Bidi Bidi nchini Uganda
Kambi ya wakimbizi ya Bidi Bidi nchini Uganda RFI/Gaël Grilhot
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa kufungua tena kambi hiyo, umechukuliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi UNHRC na serikali ya Uganda kuwasaidia wakimbizi hao wanaoingia nchini humo kwa wingi.

Kambi hii imekuwa maarufu sana tangu mwaka 1990, kuwapa hifadhi raia wa Sudan Kusini ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikimbia nchi yao kwa sababu ya vita.

Kambi hiyo ilifungwa rasmi na serikali ya Uganda mwaka 2000 wakati wakimbizi hao waliporudi nyumbani.

Sardhanand Panchoe, afisa wa UNHCR nchini humo ameliambia Gazeti la Daily Moniter kuwa kambi hiyo itasaidia pakubwa kuwapa hifadhi maelfu ya wkaimbizi ambao wamekuwa wakiwasili katika Wilaya ya Moyo Kaskazini mwa Uganda.

Mbali na kambi hii, Uganda imewapa hifadhi maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini wanaoishi katika kambi mbalimbali katika wilaya za Adjumani, Arua na Yumbe.

Takwimu zinaonesha kuwa kambi ya Bidibidi peke yake katika Wilaya ya Yumbe ina wakimbizi 213,279 .

Wakimbizi karibu 4,000 huwasili nchini Uganda karibu kila siku wakati huu thathmini ikionesha kuwa wanakabiliwa na maisha magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.