Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA

Ufaransa kuanza tena uchunguzi dhidi ya mauaji ya kimbari ya Rwanda

Wachunguzi nchini Ufaransa wameanza tena uchunguzi wao katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda yaliyochochewa na mauaji ya rais wa Rwanda Juvenual Habyarimana,kwa kumhoji jenerali mpinzani ambaye anamtuhumu rais wa sasa wa nchi hiyo kuchochea mauaji,AFP imefahamishwa jana Ijumaa. 

Jenerali Kayumba Nyamwasa mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda
Jenerali Kayumba Nyamwasa mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda AFP PHOTO / ALEXANDER JOE
Matangazo ya kibiashara

Baada ya ndege ya Ufaransa iliyokuwa imembeba rais wa zamani wa Rwanda Juvenual Habyarimana kudunguliwa na kombora Aprili 6, 1994, kampeni kulenga jamii ya Watutsi wa Rwanda ilianza ambapo ndani ya siku 100, watu wapatao 800,000 waliuawa.

Mkuu wa zamani wa majeshi nchini Rwanda Faustin Kayumba Nyamwasa ambaye mahakimu wachunguzi wa Ufaransa wanataka kumhoji, anaishi uhamishoni nchini Afrika Kusini, ambako amenusurika majaribio takribani mawili ya kuuawa.

Kama Rais Paul Kagame, Nyamwasa alikuwa mwanachama mwanzilishi wa kundi la waasi la Rwanda Patriotic Front (RPF) ambalo baadaye lilichukua madaraka mwishoni mwa mwaka 1994, na kukomesha mauaji ya kimbari.

Katika hati iliyowasilishwa kwa wachunguzi wa Ufaransa mwezi Juni mwaka huu, Nyamwasa alikanusha ushahidi wa shuhuda ambao unamfunga kuhusika na tukio la kudungua ndege ya Habyarimana, na kusema Kagame anahusika na shambulizi, ambalo pia liligharimu maisha ya aliyekuwa rais wa Burundi.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.