Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFRIKA KUSINI

Udunguaji wa ndege ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana, Afrika Kusini haijatowa jibu la Hakimu wa Ufaransa kumuhoji Kayumba Nyamwasa

Hii ni taarifa maalum ya RFI: Tangu kipindi cha mwaka mmoja na nusu, mahakama nchini Ufaransa imeomba bila mafaanikio viongozi wa Afrika Kusini kuruhusu kumuhoji Jenerali Kayumba Nyamwasa aliye uhamishoni nchini humo kuhusu tukio la kudunguliwa kwa ndege iliokuwwemo ma rais Habyarimana wa Rwanda na Cyprien Ntaryamira wa Burundi April 6 mwaka 1994. kiongozi huyo wa zamani wa kundi la Rwanda Patriotic Front, (RPF) alithibitisha kupitia RFI mwezi Julai iliopita kuwa anaoushahidi wa kutosha unaomuhusisha rais wa Rwanda Paul Kagame katika tukio hilo na yupo tayari kutowa ushahidi kwa jaji wa Ufaransa.

Exiled Rwandan General Faustin Kayumba Nyamwasa looks on during his court appearance in Johannesburg, 21 June, 2012
Exiled Rwandan General Faustin Kayumba Nyamwasa looks on during his court appearance in Johannesburg, 21 June, 2012 Reuters/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Hakimu wa maswala ya ugaidi Marc Trévidic aliiomba kamisheni ya kimataifa kumuhoji jenerali Kayumba Nyamwasa ambaye alikuwa mkuu wa majeshi ya kundi la waasi zamani wa RPF na ambaye anaeshi uhamishoni nchini Afrika Kusini.

Kulingana na duru sahihi, tume hii ilipitishwa mwezi Aprili mwaka 2012 katika Ubalozini na kupelekwa mwezi mmoja baadaye kwa mamlaka ya Afrika Kusini. Hata hivyo ombi hilo limebaki bila majibu. Hii si mara ya kwanza kwa hakimu Trévidic kukabiliwa na kikwazo kuhusu utawala wa Afrika Kusini.

Hakimu huyo alikuwa ameomba kusafirishwa kwa Kayumba Nyamwasa . Taarifa iliothibitishwa na mwendesha mashtaka wa Ufaransa mwezi Julai 2010.

Kama mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda hajashtakiwa kwa madai ya kuhusika kwake katika shambulio dhidi ya ndege ya Rais wa zamani Juvenal Habyarimana , bado yupo chini ya waranti ya kukamatwa. Licha ya kubadili ombi la kusafirishwa na kutaka kuhojiwa kwa kiongozi huyo bado ombi hilo halijafua dafu.

Ukimya wa Pretoria.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Afrika Kusini Clayson Monyela, amejizuia kuzungumza lolote kuhusu taarifa hii na kuelekeza kwamba hili ni jukumu la wizara ya sheria kujieleza. Hata hivo msemaji wa Wizara ya Sheria alijiuzuia kuzungumza lolote na RFI.

Je! Kesi hii ilizungumzwa na Waziri wa sheria wa Ufaransa wakati wa ziara yake mapema wiki hii nchini Afrika Kusini? Christiane Taubira aliongozana na Rais Francois Hollande wakati wa ziara yake, nchini humo ambapo rais Hollande alikutana na mwenyeji wake wa Afrika Kusini.

Ubalozi wa Kifaransa naopia umejizuia kutowa maoni kuhusu kesi ambayo ipo chini ya uchunguzi. Kiongozi Mwingine wa Kifaransa amekataa kuzungumzia swala hilo na kusema kwamba muda bado upo na ombi kama hili kuwa linachukuwa muda na sio tu kwa Afrika Kusini.

Upande wa Utetezi

Mwansheria wa familia ya rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana Wakili Philippe Meilhac amesema Kayumba Nyamwasa mwenyewe alitangaza kuwa na ushahidi wa kutosha, na kwanini asisikilizwe. Kayumba Nyamwasa alithibitisha mwezi Julay iliopita kupitia mahojiano maalum na RFI kwamba anaoushahidi wa kutosha unaomuhusisha rais wa Rwanda Paul Kagame katika tukio hilo la udunguaji wa ndege iliokuwemo viongozi wa Rwanda na Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.