Pata taarifa kuu
BURUNDI-ICC

Burundi yachukua uamuzi wa kujiondoa kuwa mwanachama wa ICC

Serikali ya Burundi imechukua uamuzi wa kujiondoa kuwa mwanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya (ICC). Uamuzi huu unakuja baada ya wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kutoa orodha ya viongozi 12 serikalini ambao wanatuhumiwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu nchini Burundi. Watu hao karibu wote ni washirika wa karibu wa Rais Pierre Nkurunziza.

Kikao cha baraza la mawaziri kikiongozwa na Rais Pierre Nkurunziza, Alhamisi Oktoba 6, 2016.
Kikao cha baraza la mawaziri kikiongozwa na Rais Pierre Nkurunziza, Alhamisi Oktoba 6, 2016. © RFI-KISWAHILI
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa kujiondoa kuwa mwanacahama wa ICC ulichukuliwa katika kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika Alhamisi wiki hii.

Msemaji wa serikali ya Burundi, Philippe Nzobonariba, amewathibitishia waandishi wa habari mjini Bujumbura Alhamisi hii jioni kwamba uamuzi huo umechukuliwa na kwamba kinachosalia ni kupitishwa na Bunge pamoja na baraza la seneti.

Nchi nyingi za Afrika zimekua zikitathmini uwezekano wa kujiondoa kuwa wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Afrika.

Nchi hizi zinashtumu Mahaka hiyo kwamba inatumiwa na nchi zenye nguvu kwa kuwafunguliwa mashitaka viongozi wa nchi za Afrika.

Itafahamika kwamba maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi, polisi na baadhi ya maafisa serikalini nchini Burundi wanatuhumiwa na mashirika mbalimbali ya kimataifa ya haki za binadamu kuhusika na vitendo viovu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mauaji na mateso dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu, wanasiasa na wafuasi wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.