Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

UNSC yaitaka Sudan Kusini kukubali askari 4,000 wa ziada

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana limetoa wito kwa Sudan Kusini kuacha upinzani wake kuhusu kupelekwa kwakikosi cha kikanda cha kuimarisha ulinzi katika ujumbe wa askari wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani katika nchi hiyo inayotatizwa na vita.

Mjumbe wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power akiwasili mjini Juba 03 Sept 2016
Mjumbe wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power akiwasili mjini Juba 03 Sept 2016 www.un.org
Matangazo ya kibiashara

Wakirejea wito uliotolewa hapo awali jana Jumamosi na viongozi wa kidini wa Sudan Kusini, mabalozi kutoka nchi 15 wanachama wa baraza hilo walikutana na mawaziri waandamizi wa serikali mjini Juba na wote walizungumzia kuunga mkono pendekezo la kutumwa kwa wanajeshi 4,000 wa ziada kwa kikosi cha askari 13,000 wa UNMISS waliomo nchini humo.

Mmoja wa mabalozi, ambaye hakutaka jina lake litajwe, ameiambia AFP kuwa mawaziri wa Sudani Kusini walishangazwa kuona kwamba baraza hilo linazungumza kauli moja pamoja na China na Urusi.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Samantha Power baada ya kuwasili mjini Juba, amesisitiza kwamba askari 4,000 wa ziada wa kulinda amani kutoka Afrika wanahitajika.

Hata hivyo Serikali ya Sudan Kusini inapinga mapendekezo ya kupelekwa kwa askari wa ziada wa kulinda amani nchini humo kwa madai kwamba hatua hiyo inakiuka uhuru wa nchi hiyo kujitawala.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.