Pata taarifa kuu
DRC

FARDC na MONUSCO wazidisha mashambulizi dhidi ya ADF; Mazungumzo shakani

Vikosi vya jeshi la Congo vya FARDC vimefaulu kuisambaratisha ngome ya waasi wa Uganda wa ADF waliopiga kambi nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika kijiji cha Mwalika kusini mashariki mwa mji wa Beni Mkoani Kivu ya Kusini. 

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa MONUSCO na wale wa Serikali ya DRC, FARDC wakikagua moja ya ramani inayoonesha maeneo ambayo kundi la ADF Nalu limepiga kambi, hii ilikuwa mwake 2014.
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa MONUSCO na wale wa Serikali ya DRC, FARDC wakikagua moja ya ramani inayoonesha maeneo ambayo kundi la ADF Nalu limepiga kambi, hii ilikuwa mwake 2014. UN Photo/Sylvain Liechti
Matangazo ya kibiashara

Duru za kijeshi zinaeleza kwamba kundi hilo la waasi wa ADF liliweka ngome yake katika bonde la Malika tangu Julay 25 pale wanajeshi wa FARDC walipoanza operesheni ya kuwasaka waasi hao katika eneo lilibatizwa Triangle of Death lililopo kati ya Mbau-Kamango na Erengeti.

Hata hivyo shirika la CEPADHO linalo tetea haki za binadamu linaeleza kwamba vikosi vya FARDC vimeudhibiti mji huo wa mwalika bila mapambano, ambapo waasi wa ADF walipata muda wa kuondoka katika eneo hilo kabla ya ujio wa jeshi.

Mashirika ya kiraia katika mji wa Beni yamepongeza juhudi za jeshi la FARDC na kuwatolea wito kuendelea zaidi kumsaka adui ambae wanaona kwa sasa amesambaratika, hivyo ni fursa ya kumtokomeza kwa kutompa nafasi ya kujipanga upya.

Katika hatua nyingine, mchakato wa mazungumzo ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umeendelea kusuasua wakati huu baadhi ya wanasiasa nchini humo hususan wa upinzani wakigawanyika kuhusu mazungumzo hayo ambayo baadhi wanaona kwamba hayana tija yoyote.

Rais Joseph Kabila aliitisha mazungumzo hayo ili kuzungumzia mustakabali wa taifa hilo kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, lakini upinzani wao waona hizi ni njama zake za kutaka kuendelea kusalia madarakani sababu katiba haimruhusu tena kuwania urais.

Jumuiya ya Kimataifa inaunga mkono mazungumzo hayo ambayo inaona ndio njia pekee ya kuondokana na mzozo wa kisiasa uliopo.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa maziwa makuu SAIDI DJINNIT anasema wanaendelea na mashauriano na pande zote husika na mzozo huo wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.