Pata taarifa kuu
DRC-MONUSCO-SIASA-USALAMA

DRC: Monusco yawataka wanasiasa kuheshimu Katiba ya nchi

Maafisa wa tume ya umoja wa mataifa nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Monusco wamewataka viongozi wa nchi hiyo na wanasiasa wengine kuhakikisha kuwa katiba ya nchi hiyo inaheshimiwa.

Joseph Kabila, le 3 février 2015.
Joseph Kabila, le 3 février 2015. AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa Jumatano wiki hii, msemaji wa tume hiyo, Prosper Felix Bass amesema Monusco imeridhishwa na hatua ya wanasiasa saba waliojitokeza na kumwandikia barua rais Joseph Kabila Kabange kuhakikisha uchaguzi wa urais unafanyika chini ya misingi ya kidemokrasia katika muda uliopangwa, mwezi novemba mwaka ujao.

Bass amesema wimbi la kisiasa lililopo hivi sasa nchini DRCongo limedhihirisha kuwa kuna dalili ya kuwepo kwa matukio mabaya zaidi endapo serikali ya nchi hiyo itakaidi malalamiko ya wanasiasa hawa.

Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Joseph Kabila amewafuta viongozi wakuu wawili katika Serikali yake, saa chache baada ya wanasiasa hao kumuandikia barua ya wazi wakimuonya kuhusu azma yake ya kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Viongozi hao wakuu ni pamoja na mshauri wa masuala ya usalama, Pierre Lumbi, pamoja na waziri wa mipango, Olivier Kimatatu, kwenye orodha hiyo wamo pia wanasiasa wengine watano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.