Pata taarifa kuu
Kenya

Afisa mmoja wa polisi auawa nchini Kenya huku wengine kumi wakijeruhiwa katika mlipuko wa guruneti jijini Mombasa

Afisa mmoja wa polisi nchini Kenya ameuawa huku wengine zaidi ya kumi wakijeruhiwa  mapema leo asubuhi katika mlipuko wa guruneti uliotokea wakati polisi walipokuwa wakiendesha msako katika nyumba moja jijini Mombasa.

Polisi wa Kenya wakiwa katika msako jijini Mombasa
Polisi wa Kenya wakiwa katika msako jijini Mombasa Reuters/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa polisi katika eneo hilo Aggrey Adoli amethibitisha kutokea kwa mlipuko huo ambao amesema huenda umeendeshwa na watu wenye uhusiano na wapiganaji wa kundi la Al Shabab. 

Hata hivyo polisi walifaanikiwa kumuuwa mshambuliaji mmoja na mwingine aliuawa wakati alipojilipua na guruneti. Msakao huo uliendeshwa katika eneo la Likoni karibu na bandari ya Mombasa baada ya kupewa taarifa za kuwepo kwa wapiganaji katika eneo hilo. Bunduki mbili, guruneti na risase vimakamatwa katika msako huo.

Polisi nchini Kenya imeanzisha operesheni ya kuwasaka wafuasi wa kundi la Mombasa Republican Concil MRC, kundi ambalo linataka eneo la Mombasa kujitenga na serikali ya Kenya na kuitewa serikali huru. Watu wawili waliuawa jumatatu wakati wa operesheni ya kumkamata kiongozi wa kundi hilo la MRC Omar Mwamunwadzi.
Aggrey Adoli amesema kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya operesheni ya leo na kundi la MRC.

Wafuasi wa kundi la Al Shabab wenye mafungamano na Alqaeda, siku za nyuma waliendesha mashambulizi dhidi ya polisi wa Kenya katika eneo la Mombasa, linalo hudhuriwa na watalii wengi kutoka nchi za kigeni na maeneo mengine ya Kenya pia yalisham,buliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.