Pata taarifa kuu
Uholanzi

ICC yamkuta na hatia kiongozi wa majeshi ya waasi nchini Congo, Thomas Lubanga

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita,ICC hii leo imemkuta na hatia ya makosa ya Uhalifu wa kivita kiongozi wa Jeshi la waasi nchini Congo, Thomas Lubanga. 

Kiongozi wa Majeshi ya waasi nchini Congo, Thomas Lubanga
Kiongozi wa Majeshi ya waasi nchini Congo, Thomas Lubanga (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Lubanga menye umri wa miaka 51 alikutwa na hatia ya kuwasajili watoto katika jeshi lake na kuwatumia katika mapambano wakati wa miaka minne ya vita nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vita vilivyomalizika mwaka 2003.

Mahakama hiyo imefikia uamuzi wake kuwa Mashtaka hayo yamedhihirisha kuwa Lubanga ana hatia ya kuwaita jeshini watoto wenye umri wa chini ya miaka 15
na kuwatumia katika mapigano.

Waendesha mashtaka wameiambia Mahakama kuwa watoto wenye umri wa miaka 11 walikuwa wakichukuliwa kutoka majumbani mwao, shuleni na katika viwanja vya michezo ili kulitumikia jeshi la Lubanga huku watoto wa kike wakitumikishwa katika vitendo vya Ngono.

Makundi ya watu wanaottea haki za Binaadam yamesifu uamuzi wa Mahakama, kwa kusema kuwa unatoa Ujumbe kwa viongozi wa wanaoshurutisha watoto kupigana vita akiwemo kiongozi wa waasi wa Uganda, Joseph Kony.

Lubanga anakabiliwa na kifungo cha mpaka Miaka 30 jela au kifungo cha Maisha Jela, hata hivyo Lubanga ana siku 30 za kukata rufaa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.