Pata taarifa kuu

Tanzania: Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi afariki dunia akiwa na umri wa miaka 98

Rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, ambaye alianzisha demokrasia ya vyama vingi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, amefariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 98, ofisi ya rais imetangaza.

Rais wa pili wa Tanzania Hassan Mwinyi (wa pili kulia) akihudhuria misa ya kuaga mwili wa marehemu Rais wa Tanzania John Magufuli kabla ya kuzikwa kwenye Uwanja wa Magufuli mjini Chato, Tanzania, Machi 26, 2021.
Rais wa pili wa Tanzania Hassan Mwinyi (wa pili kulia) akihudhuria misa ya kuaga mwili wa marehemu Rais wa Tanzania John Magufuli kabla ya kuzikwa kwenye Uwanja wa Magufuli mjini Chato, Tanzania, Machi 26, 2021. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Nina huzuni kutangaza kifo hiki," amesema Rais Samia Suluhu Hassan, na kuongeza kuwa rais huyo wa zamani alikuwa akitibiwa saratani ya mapafu. Mwinyi alilazwa London Novemba 2023 kabla ya kurejea kuendelea na matibabu Dar es Salaam, ameongeza Rais wa Tanzania.

Serikali imetangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa, huku bendera za taifa zikiwa nusu mlingoti. Aliyechaguliwa na shujaa wa uhuru Julius Nyerere kurithi nafasi yake, Mwinyi alirithi nchi iliyokuwa kwenye mtikisiko wa uchumi, baada ya miaka mingi ya majaribio ya wasoshalisti kushindwa.

Aliondoa vikwazo kwa makampuni binafsi na kupunguza vikwazo vya uagizaji bidhaa kutoka nje, na kumpatia jina la utani "Mzee Rukhsa", msemo wa Kiswahili ambao unaweza kutafsiriwa kama "Ruhusa ya Mheshimiwa".

Alizaliwa Mei 8, 1925 katika koloni la zamani la Waingereza lililojulikana kwa jina la Tanganyika, Mwinyi alihamia Zanzibar kusoma Uislamu. Baba yake alitarajia angekuwa kiongozi wa kiroho, lakini kijana Mwinyi badala yake aligeukia ualimu, kabla ya kuingia kwenye siasa miaka ya 1960, baada ya ukombozi wa Tanganyika.

Kufuatia muungano wa Tanganyika na Zanzibar huru mwaka 1964 na kuunda Tanzania, alipanda ngazi hadi kuwa balozi nchini Misri na pia waziri wa afya, waziri wa mambo ya ndani na waziri wa maliasili katika miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980. Mwaka 1984, akawa rais. wa Zanzibar, kabla Nyerere hajamchagua kuiongoza Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.