Pata taarifa kuu

Watu 25 wamefariki katika ajali ya barabarani nchini Tanzania

Nairobi – Nchini Tanzania, mwishoni mwa wiki iliyopita, ajali mbaya ajali ya barabarani iliyohusisha magari manne katika eneo la Kibaoni- Ngaramtoni mjini Arusha imesababisha vifo vya watu 25, wakiwemo raia wa Kigeni kutoka Kenya, Marekani na Afrika Kusini.

Karibia watu 21 kutoka mataifa tofauti ya kigeni waliripotiwa kujeruhiwa katika ajali hiyo
Karibia watu 21 kutoka mataifa tofauti ya kigeni waliripotiwa kujeruhiwa katika ajali hiyo © https://wwwnc.cdc.gov/
Matangazo ya kibiashara

Mmoja ya magari iliyohusika kwenye ajali hiyo, ilikuwa inawasafirisha raia wa kigeni waliokuwa wanafanya kazi ya kujitolea kwenye shule moja mjini Arusha.

Awadhi Juma Haji ni Kamishena wa Polisi wa opereseni ya mafunzo wa jeshi la Polisi nchini humo, anaelezea kilichojiri.

“Waliofariki ni wanaume 14, wanawake 10 na mtoto mmoja wa kike, jumla 25.” alieleza Awadhi Juma Haji.

00:46

Awadhi Juma Haji

Ajali hiyo ilitokea baada ya lori lenye nambari ya usajili ya Kenya kugonga magari matatu likiwemo moja lililokuwa linawasafirisha raia wa kigeni waliokuwa wanafanya kazi ya kujitolea.

Karibia watu 21 kutoka mataifa tofauti ya kigeni waliripotiwa kujeruhiwa katika ajali hiyo.

Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na raia wa Marekani, Afrika Kusini na wengine kutoka nchi za Kenya, Togo, Madagascar na Burkina Faso.

Waliojeruhiwa ni kutoka nchi za Nigeria, Ivory Coast, Cameroon, Switzerland, Uingereza na Mali, kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka.

Rais Samia Hassan ametuma pole zake kwa walioathirika na familia zilizowapoteza watu wao kwenye ajali hiyo.

Polisi kwenye taifa hilo wanaendelea na juhudi za kumsaka dereva wa lori hilo ambalo lilisababisha ajali ambaye anadaiwa kutoweka baada ya ajali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.