Pata taarifa kuu

Tanzania: Ukosefu wa sukari wazua hali ya wasiwasi

Nairobi – Kukosekana kwa sukari nchini Tanzania kumezua hali ya wasiwasi kwa wananchi ambapo licha ya bidhaa hiyo kuwa adimu, baadhi ya wafanyabiashara wanalalamikiwa kuhodhi na kuuza kinyume na bei elekezi iliyotolewa na Serikali, hali ambayo inazidisha ukali wa maisha.

Kukosekana kwa sukari nchini Tanzania kumezua hali ya wasiwasi kwa wananchi
Kukosekana kwa sukari nchini Tanzania kumezua hali ya wasiwasi kwa wananchi DR
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku za usoni nchini Tanzania kumeripotiwa uwepo wa uhaba wa sukari jambo linalo waumiza sio tu wafanyabaishara wa maduka ya jumla na rejareja nchini humo bali pia Mama lishe ambao hutegemea kwa sehemu kibwa bidhaa hii muhimu.

“Tunapataka changamoto katika uuzaji wa chai, chai inabaki maana wateja wamepungua.” alieleza mkaazi wa Tanzania.

00:05

Mfanyibiashara nchini Tanzania

Katika kupambana na walaguzi wa sukari serikali katika pembe mbalimbali nchini Tanzania kupitia viongozi wake imekuwa ikifanya ziara katika maduka makumbwa, Amina Makilagi ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.

“Mkuu wa mkoa alitoa maelekezo kwamba tujitahidi kuhakikisha tunadhibiti sukari ilikisiswe ni kiwango ambacho hakijaelekezwa na serikali.” alisema Amina Makilagi ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.

00:11

Amina Makilagi ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana

Nchini Tanzania kiwango cha uzalishaji sukari kimeongezeka kutoka miaka ya 1970, lakini bado haijitosheleza kwa mahitaji, ambapo kwa kwa sasa mahitaji ya sukari ni tani 686,000 kwa mwaka.

Martin Nyoni Mwanza- RFI Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.