Pata taarifa kuu

Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa afariki dunia

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa afmeariki dunia. Kwa muda mrefu alikuwa akitibiwa nchini Afrika Kusini, amefariki dunia Jumamosi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyoko jijini Dar es salaam. 

Edward Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953 amefariki akiwa na umri wa miaka 70 na anaacha alama kama moja ya miamba ya siasa za Tanzania.
Edward Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953 amefariki akiwa na umri wa miaka 70 na anaacha alama kama moja ya miamba ya siasa za Tanzania. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

 

 

Katika tangazo fupi alilolitoa kupitia televisheni ya taifa,  Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango, amesema kuwa Lowassa amefikwa na umauti katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

''Amefariki leo akipatiwa matibabu kwa ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu. Hayati Ngoiyai Lowassa ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu tarehe 14 mwezi Januari mwaka 2022''. Alisema Dkt. Mpango

"Amefariki dunia  leo wakati akipatiwa matibabu kwa ugonjwa wa kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu. Lowassa ameugua kwa muda mrefu  na amekuwa akipatiwa matibabu,” alisema makamu huyo wa rais.

Alikuwa akipatiwa matibabu katika taasisi hiyo ya moyo kisha kupelekwa Afrika Kusini na baadaye kurudishwa tena katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.

Lowassa alihudumu kama Waziri Mkuu wa Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa miaka mitatu, toka 2005 mpaka 2008 alipolazimika kujiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond.

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo hicho akimwelezea kiongozi huyo kuwa ni miongoni mwa watu wa kukumbukwa nchini Tanzania huku akitangaza siku tano za maombolezo.

 "Tumempoteza kiongozi mahiri, aliyejituma na kujitoa kwa nchi yetu..." ameandika Rais Samia katika ukurasa wake wa X.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia hii leo.

Alikuwa waziri mkuu kati ya mwaka 2005 hadi 2008 chini ya uongozi wa rais Jakaya Kikwete. Alizaliwa Agosti 26, 1953 na wakati wa uhai wake alikuwa  mbunge wa Jimbo la Monduli mkoani Arusha kwa tiketi ya CCM.

Alikuwa mwanasiasa aliyekubalika na kupendwa wa wengi na baadhi walimtazama kama kiongozi ambaye angeliweza kupeperusha bendera ya chama chake katika uchaguzi wa mwaka 2015.  Hata hivyo, chama chake kilimtupa mkono hatua ambayo ilimfanya kujiunga na chama cha upinzani Chadema na kuleta ushindani mkubwa katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Lowassa hata hivyo alishindwa katika uchaguzi huo na aliyekuwa mgombea wa CCM John Pombe Magufuli. Lowassa alirejea CCM mwaka 2019.

Lowassa alizaliwa Agosti 26, 1953 amefariki akiwa na umri wa miaka 70 na anaacha alama kama moja ya miamba ya siasa za Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.