Pata taarifa kuu

Tanzania: Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amefariki

Nairobi – Waziri mkuu wa zamani nchini Tanzania Edward Lowassa amefariki dunia wakati akipokea matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.

Kifo chake kimethibitishwa na makamu wa rais, Dkt. Philip Mpango
Kifo chake kimethibitishwa na makamu wa rais, Dkt. Philip Mpango REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Kifo chake kimethibitishwa na makamu wa rais, Dkt. Philip Mpango.

Lowassa alihudumu katika nafasi ya waziri mkuu kati ya mwaka 2005 hadi 2008 chini ya uongozi wa rais wa zamani Jakaya Kikwete.

Mwaka wa 2015 aliwania urais kwenye uchaguzi mkuu akiwa mgombea wa chama cha (CHADEMA) ambapo alishindwa na aliyekuwa rais hayati John Magufuli.

Serikali imetangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo Jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.