Pata taarifa kuu

Tanzania: Chama kikuu cha upinzani kimeandaa maandamano Dar es Salaam

Nairobi – Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, kimeandaa maandamano ya amani hivi leo jijini Dar es Salaam, ambayo yameruhusiwa na polisi kudai mageuzi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka ujao.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA akiwahotubia wafuasi wa chama hicho jijini Mwanza, Januari 21 2023
Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA akiwahotubia wafuasi wa chama hicho jijini Mwanza, Januari 21 2023 © Martin Nyoni
Matangazo ya kibiashara

Chadema imesema kibali cha kushiriki maandamano hayo kimetolewa kufuatia makubaliano na polisi kuruhusu maandamano ya amani.

Tangu alipochukua hatamu za uongozi, rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiruhusu vyama vya upinzani, kushiriki kwenye mikutano ya kisiasa kinyume na ilivyokuwa hapo awali.

Kwa mujibu wa Chadema, maandamano ni ya kupinga mapendekezo ya miswada ya sheria ya uchaguzi, gharama kubwa ya maisha na kucheleweshwa kwa marekebisho ya katiba.

Chama hicho kilisema kitaongoza maandamano hayo Jumatano ili kuishinikiza serikali kutekeleza mageuzi hayo kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Uchaguzi wa serikali za mitaa umepangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Haya yatakuwa ni maandamano ya kwanza kufanyika nchini tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani Machi 2021 kufuatia kifo cha mtangulizi wake John Magufuli.

Magufuli alikuwa akishutumiwa kwa kukandamiza upinzani baada ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.