Pata taarifa kuu

Tanzania: Mafuriko yashuhudiwa jijini Dar es Salaam

Nairobi – Nchini Tanzania, watu kadhaa wameripotiwa kufariki, nyumba na barabara zikiharibiwa baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko katika mji wa kibiashara Dar es Salaam kwa muda wa siku mbili.

Ramani ya nchi ya Tanzania
Ramani ya nchi ya Tanzania © https://wwwnc.cdc.gov/
Matangazo ya kibiashara

Nyumba kadhaa zilizo karibu na mto zilianguka, barabara na daraja zikiharibiwa hatua ambayo imefanya kuwa vigumu kwa watu kusafiri.

Barabara kuu ya Bagamoyo inayounganisha jiji kuu na maeneo ya kaskazini mwa taifa hilo haikuwa inapitika siku ya Jumapili baada ya mvua kubwa kunyesha kwenye eneo hilo.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu siku ya Jumapili aliwataka raia kuchukua tahadhari kwa kuepuka maeneo hatari.

Aidha mkuu wa nchi ametoa wito kwa mamlaka ya uokozi kuhakikisha kuwa mvua inayoendelea kunyesha haisababishi vifo.

Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki imeonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa mvua kubwa mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.