Pata taarifa kuu

Mashariki mwa DRC: Kikosi cha kikanda cha Afrika Mashariki chaanza kuondoka

Kikosi cha kikanda cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-RF), ambacho Kinshasa imeamua kutokiongezea muda wa kuhudumu Mashariki mwa DRC, kimeanza kuondoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumapili asubuhi, vyombo vya habari vimeripoti.

Msemaji wa EAC-RF kwenye amethibitisha kuwa ndege hiyo imeelekea Nairobi na imebeba wanajeshi wa Kenya pekee, lakini hakutoa maelezo zaidi mara moja juu ya muendelezo wa kuondoka kwa kikosi hicho.
Msemaji wa EAC-RF kwenye amethibitisha kuwa ndege hiyo imeelekea Nairobi na imebeba wanajeshi wa Kenya pekee, lakini hakutoa maelezo zaidi mara moja juu ya muendelezo wa kuondoka kwa kikosi hicho. © Florence Morice / RFI
Matangazo ya kibiashara

Kundi la kwanza la takriban wanajeshi mia moja wa Kenya kutoka katika kikosi hicho, ambacho pia kinajumuisha wanajeshi wa Uganda, Burundi na Sudan Kusini, wameondoka eneo hilo kutoka uwanja wa ndege wa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, kuelekea Nairobi.

Ndege yao imeondoka muda mfupi baada ya 5:00 Alfajiri kwa saa za Afrika ya Kati.

Msemaji wa EAC-RF kwenye amethibitisha kuwa ndege hiyo imeelekea Nairobi na imebeba wanajeshi wa Kenya pekee, lakini hakutoa maelezo zaidi mara moja juu ya muendelezo wa kuondoka kwa kikosi hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.