Pata taarifa kuu

DRC haitaongeza muda wa kikosi EAC eneo la mashariki

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeendelea kushikilia msimamo wake wa kukitaka Kikosi cha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoongezewa muda wa kuhudumu eneo la mashariki mwa nchi hiyo baada ya muda huo kutamatika Desemba 08 2023.

Kinshasa inawatuhumu wanajeshi wa EAC kwa kushindwa jukumu lao la kurejesha usalama mashariki mwa nchi
Kinshasa inawatuhumu wanajeshi wa EAC kwa kushindwa jukumu lao la kurejesha usalama mashariki mwa nchi AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Hili lilithibitishwa na waziri wa ulinzi wa DRC Jean pierre Bemba wakati wa mkutano wa 23 wa viongozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki, EAC .

Viongozi hao waliktana katika mkutano wa kilele nchini Tanzania, jijini Arusha, Ijumaa hii Novemba 24, ambapo miongoni mwa wakuu wa nchi waliohudhuria ni pamoja na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, Salva Kiir, Wa Sudan Kusini, ambaye anachukua uenyekiti na hivyo kurithi nafasi ya Rais wa Burundi Evariste Ndayisihimye.

Hata hivyo rais wa Rwanda Paul Kagame naye Félix Thisekedi wa DRC hawakuhudhuria mkutano huo ambao pamoja na kuikubalia nchi ya Somalia kuwa mwanachama mpya wa Jumuia ya Afrika mashariki huku Jumuya hiyo yenye nchi wanachama wanane sasa ikitafuta kupanua biashara huria katika kanda hiyo.

Wakuu hao wa EAC pia walijadiliana kuhusu hali ya mashariki mwa DRC, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zaidi za  kukomesha mapigano yanayoendelea mkoani Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. 

M23 wamekuwa wakikabiliana na wanajeshi wa DRC katika mji wa Mweso
M23 wamekuwa wakikabiliana na wanajeshi wa DRC katika mji wa Mweso © Glody Murhabazi / AFP

Nchi saba za eneo hilo, wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, zilituma vikosi vyao mashariki mwa DRC mara ya kwanza Novemba 2022 baada ya kuchipuza tena kwa kundi la waasi la M23. 

Taarifa ya jumuiya ya EAC iliyotolewa baada ya kongamano jijini Arusha ijumaa ya Novemba 24 ilisema kwamba viongozi wa nchi hizo wamekubaliana kuongeza juhudi za pamoja ili kupatanisha majirani DRC na Rwanda licha ya kuwa serikali ya Kinshasa ilikuwa imesema muda wa kikosi cha EACRFutaendelea hadi Disemba 8, ikisubiriwa ripoti ya tathmini ya kazi ya kikosi hicho. 

DRC imekuwa ikiituhumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 suala ambalo kigali imeendelea kukana
DRC imekuwa ikiituhumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 suala ambalo kigali imeendelea kukana © AFP - SIMON WOHLFAHRT

Hali ya kikosi hicho cha pamoja nchini Congo imekuwa ikitiliwa shaka hasa baada ya Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi kukikosoa lakini EAC iliamua mwezi Juni kukiacha kikosi hicho nchini humo kwa miezi mitatu zaidi. 

Somalia ambayo Rais wake Hassan Sheikh Mohamud alikuwa kwenye mkutano wa Ijumaa, inaungana na Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda. 

Jumuia ya Afrika Mashariki yenye makao yake makuu mjini Arusha ambako mkutano huo ulikuwa unafanyika, ilianzishwa mwaka 2000, na inahusika na kuhimiza biashara kwa kuondoa ushuru wa forodha baina ya nchi wanachama. Ilianzisha soko la pamoja mwaka wa 2010. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.