Pata taarifa kuu

DRC : Masuala ambayo raia watazingatia kabla ya kumchagua rais mpya

Nairobi – Wakati huu raia wa DRC wakijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwezi ujao na wagombea wa nafasi mbalimbali kuendelea kunadi sera zao, utendakazi unatarajiwa kuwa kipimo kwa rais Felix Tshisekedi, anayetaka kuchaguliwa kwa muhula wa pili.

Rais Felix Tshisekedi, anayetaka kuchaguliwa kwa muhula wa pili, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wanasiasa wa upinzani
Rais Felix Tshisekedi, anayetaka kuchaguliwa kwa muhula wa pili, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wanasiasa wa upinzani Sumy Sadurni / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya maswala ambayo yatazingatiwa na wapiga kura, ni pamoja na hali  ya kiuchumi nchini humo ambapo licha ya nchi hiyo kuwa na raslimali za kutosha ikiwemo madini, kiwango cha umaskini kiko kwenye asilimia 62 kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2020 ya shirika la Notre Dame Global Adaptation Index.

Raia katika miji mbalimbali nchini DRC kama vile  Lubumbashi, wamekuwa wakikabiliwa na ongezeko la bei za bidhaa
Raia katika miji mbalimbali nchini DRC kama vile Lubumbashi, wamekuwa wakikabiliwa na ongezeko la bei za bidhaa AFP - FEDERICO SCOPPA

Aidha, kupanda kwa gharama ya maisha na kushuka kwa thamani ya Faranga ya Kongo ni jambo lingine ambalo raia watazingatia wakati wa kupiga kura.

Usalama, haswa mashariki mwa nchi ambako makundi ya waasi kama vile ADF, CODECO na M23 yameendelea kuwahangaisha raia ni jambo nyeti linalogusa raia wakati huu wakiwa hawajaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali kudhibiti usalama.

Makundi ya watu wenye silaha yameendelea kutatiza usalama wa raia mashariki mwa DRC
Makundi ya watu wenye silaha yameendelea kutatiza usalama wa raia mashariki mwa DRC AP - Moses Sawasawa

Kadhalika, suala la rushwa, pia linatazamwa ambapo wakosoaji wanaona ni tatizo lililokuwa sugu katika taasisi za uma nchini humo, moja ya sera ambayo inatumika na wapinzani wa Thsisekedi kuonesha ameshindwa kazi.

Suala la mwisho ni ikiwa tume ya uchaguzi nchini humo pamoja na Serikali, zitaweza kuandaa uchaguzi ulio huru, haki na kuaminika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.