Pata taarifa kuu

Kumi na tano wafariki kutokana na mafuriko nchini Kenya

Takriban watu 15 wamekufa nchini Kenya kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Afrika Mashariki, na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa hususan barabara nyini hazipiti, nyumba nyingi zimesombwa na mifugo imeangamia, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema Jumatatu.

Mvua za msimu wa mvua katika Pembe ya Afrika huchochewa na mfumo wa hali ya hewa ya El Niño.
Mvua za msimu wa mvua katika Pembe ya Afrika huchochewa na mfumo wa hali ya hewa ya El Niño. © Gideon Maundu / AP
Matangazo ya kibiashara

"Kufikia jana (Jumapili), kaya 15,264 zimeathirika, huku majeruhi 15 wakiripotiwa na angalau mifugo 1,067 imeangamia," limeandika Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya kwenye X (zamani ikiitwa Twitter).

Mvua wakati wa msimu wa mvua wa mwezi Oktoba hadi mwezi Desemba katika Pembe ya Afrika inachochewa mwaka huu na mfumo wa hali ya hewa ya El Niño, hali ya hewa inayohusishwa kwa ujumla na ongezeko la joto, ukame katika baadhi ya maeneo ya dunia na mvua kubwa katika maeneo mengine.

Mafuriko yamesababisha vifo vya watu 20 na wengine 12,000 kupoteza makazi katika jimbo la Somalia, mashariki mwa Ethiopia, serikali ya jimbo hulo ilitangaza siku ya Jumamosi. Katika nchi jirani ya Somalia, watu 14 wamekufa na karibu 114,000 wametoroka makazi yao tangu kuanza kwa msimu wa mvua, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA).

Nchini Kenya, mvua kubwa imeathiri eneo la Kaskazini hasa maeneo kame. Picha zilizorushwa katika vyombo vya habari vya eneo hilo zimeonyesha mafuriko ya maji yakipita katika vijiji, na kusababisha wakazi kukimbilia maeneo ya juu. Video nyingine pia ilionyesha helikopta ya kiraia ikiwaokoa abiria waliokuwa wamejikinga kutoka kwa paa la lori lililokwama kwenye maji katika kaunti ya Samburu, takriban kilomita 300 kaskazini mwa mji mkuu Nairobi.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Kenya ilionya wiki jana kwamba mvua kubwa "huenda ikaambatana na upepo mkali", ambao "unaweza kung'oa paa, kung'oa miti na kusababisha uharibifu wa miundo".

Pembe ya Afrika ni moja wapo ya maeneo yaliyo hatarini zaidi kwa mabadiliko ya tabianchi na hali mbaya ya hali ya hewa inatokea kwa kuongezeka kwa mzunguko na kwa nguvu kubwa mito.

Tangu mwishoni mwa 2020, Somalia pamoja na sehemu za Ethiopia na Kenya zimekumbwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika ukanda huo katika kipindi cha miaka 40. Mwishoni mwa mwaka wa 2019, takriban watu 265 walikufa na makumi ya maelfu ya wengine walikimbia makazi yao wakati wa miezi miwili ya mvua zisizokoma katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki (Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.