Pata taarifa kuu

Tabianchi Afrika: Tofauti zajitokeza kati ya marais juu ya kukuza nishati ya kijani

Wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akibaini kwamba Afrika inaweza kuwa "nguvu ya nishati mbadala" na Umoja wa Falme za Kiarabu kutangaza dola bilioni 4.5 katika uwekezaji wa nishati safi katika bara hilo, viongozi kadhaa wa mataifa ya Afrika walionyesha tofauti zao juu ya mkakati wa kupitisha juu ya suala hilo, katika siku ya pili ya mkutano wa Kilele kuhusu tabianchi barani Afrika ulioandaliwa jijini Nairobi, Septemba 5, 2023.

Rais wa Comoro na Rais wa Umoja wa Afrika Azali Assoumani akihutubia viongozi wakati wa mkutano wa Kilele kuhusu tabianchi barani Afrika mwaka 2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi, Septemba 5, 2023.
Rais wa Comoro na Rais wa Umoja wa Afrika Azali Assoumani akihutubia viongozi wakati wa mkutano wa Kilele kuhusu tabianchi barani Afrika mwaka 2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi, Septemba 5, 2023. AFP - LUIS TATO
Matangazo ya kibiashara

"Nishati mbadala inaweza kuwa muujiza wa Kiafrika. » Hivi ndivyo Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametangaza mnamo Septemba 5, 2023 kutoka jukwaa la mkutano wa kwanza wa hali ya hewa wa Afrika, huko Nairobi.

Mkutano kuhusu tanianchi barani Afrika unachukua siku tatu na utamalizika kesho Jumatano. Lengo lililotangazwa na nchi 54 za bara hilo ni kuonyesha umoja katika mapambano dhidi ya ongezeko la joto duniani, hasa katika njia zinazotekelezwa.

Lakini, kwa sasa, mataifa ya bara hili yanajaribu kuangazia sifa zao maalum na uwezo wao wa kupata ufadhili.

Katika aina hii ya mkutano wa kilele, mazungumzo huvutia hadi dakika ya mwisho. Mkutano wa jana jioni wa kuwasilisha rasimu ya tamko la mwisho hivyo ulisababisha migawanyiko mingi. Mgawanyiko ambao umeshuhudiwa tena leo Jumanne wakati wa hotuba za wakuu wa nchi.

Rais wa Jamhuri ya Kongo, Denis Sassou-Nguesso, amebaini kwamba kiini cha mapambano ya kupata ufadhili na uundaji wa soko la kimataifa la kaboni lazima liwe karibu na misitu ya Bonde la Kongo, Indonesia na Brazil. "Mabonde hayo matatu yanazingatia 80% ya bayoanuwai duniani na yanajumuisha mdhibiti wa usawa wa kaboni duniani," amesema.

Naye rais wa visiwa vya Comoro, Azali Assoumani, anataka kuwepo kwa dhana ya uchumi wa bluu ambayo huamua jukumu la bahari kuangaziwa. "Tunatetea uungwaji mkono kwa uchumi endelevu wa bluu na wito wa ushirikiano mpya na ushirikiano," amesema.

Macky Sall, rais wa Senegal, anabaini kama mwenyeji wake, Rais wa Kenya William Ruto, kwamba maendeleo ya uchumi wa kijani ndio kiini cha vita lakini kwamba ahadi za kimataifa za ufadhili hazizingatiwi. "Nchi za Kiafrika zinatekeleza miradi yao ya kijani kibichi kwa kugeukia madeni wakati ufadhili wa kukabiliana na hali hiyo unapaswa kuungwa mkono na michango, kwa mujibu wa ahadi zilizokubaliwa katika mikataba kuhusu tabianchi ya Paris," amesisitiza.

Tamko la mwisho la mkutano huu wa Nairobi litatolea siku ya Jumatano asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.