Pata taarifa kuu

DRC yakanusha kuundwa kwa Kamati ya kumfanyia kampeni rais Tshisekedi

Baadhi ya Magazeti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Alhamisi yamechapisha taarifa za rais Felix Thisekedi kutangaza kamati ya kampeni kuelekea uchaguzi wa Desemba, lakini Ikulu ya rais jijini Kinshasa imekanusha.

Félix Tshisekedi (Kulia) na Vital Kamerhe (Kushoto)wakiwa kwenye kampeni mwaka 2018
Félix Tshisekedi (Kulia) na Vital Kamerhe (Kushoto)wakiwa kwenye kampeni mwaka 2018 John WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tina Salama msemaji wa rais Tshisekedi, amezungumza na RFI Kiswahili na kuthibitisha kuwa, Kamati hiyo haijatangazwa na ripoti zilizotolewa sio sahihi.

 “Kamati ya kampeni bado haijatangazwa. Bado tunasubiri, itangazwe na rais katika siku zijazo. Hiyo Kamati haipo kwa sasa,” amesema Tina.

Aidha, Tina amesema ripoti zilizochapishwa hapo awali, hazikueleweka akiongeza kuwa, rais Tshisekedi mwenyewe atatoa tangazo hilo .

Awali, Shirika la Habari la l’Agence Congolaise de Presse (ACP), liliripoti kuwa rais Tshisekedi, alikuwa ameunda kamati ya kimkakati kumsaidia kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili.

François Muamba mkuu wa kitengo cha rais anayeshughulikia masuala ya kimkakati katika Ofisi ya rais , amenukuliwa na Shirika hilo la Habari akisema, “Kamati hiyo itatumwa katika maeneo 11 ya nchi hiyo, pamoja na mikoa 26 na Wilaya 145 pamoja na miji 36,”.

Nalo Gazeti la L’Avenir, limemnukuu Augustin Kabuya,  Katibu Mkuu wa chama cha rais Tshisekedi cha UDPS akikanusha uwepo wa Kamati hiyo.

Kabuya,  ameeleza kuwa kulikuwa na changamoto ya mawasiliano, kuhusu kutangazwa kwa Kamati hiyo ya kampeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.