Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Rais wa Sudan Kusini atuhumiwa kukiuka makubaliano ya amani

Kundi la wabunge wa chama tawala nchini la Sudan Kusini waliondoka bungeni siku ya Jumatatu, wakimtuhumu rais Salva Kiir kwa kukiuka makubaliano ya amani baada ya kupitisha sheria yenye utata ya uchaguzi.

Rais Salva Kiir mjini Juba, Februari 3, 2023.
Rais Salva Kiir mjini Juba, Februari 3, 2023. AP - Gregorio Borgia
Matangazo ya kibiashara

Mgogoro huo unahusu mfumo wa uteuzi wa wabunge, wenye utata wa hali ya juu, unaotolewa na sheria mpya kwa ajili ya uchaguzi ambao utafanyika mwaka ujao. Kundi la waandamanaji lilimshutumu Spika wa Bunge, Jemma Nunu Kulba, kwa kuidhinisha nakal hiyo bila kuwapa "fursa nzuri ya kutoa maoni yao kuhusu suala hili muhimu."

"Pendekezo la kumpa rais mamlaka mapya ili kuteua wabunge zaidi ni sawa na kuondoa mamlaka na uhuru" kutoka kwa raia wa Sudan Kusini, limelaani kundi hili linalomuunga mkono Makamu wa Rais Riek Machar, mpinzani wa Rais Kiir ndani ya ndani ya uguvugu la Ukombozi wa Sudan(SPLM). "Ni kinyume na demokrasia, halifuati sheria na haliaminiki," kundi hilo limeongeza.

Baada ya kupata uhuru kutoka kwa Sudan mwaka wa 2011, Sudan Kusini ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha karibu watu 400,000 kupoteza maisha na mamilioni kuyahama makazi yao kati ya mwaka 2013 na 2018. Mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka wa 2018 ulitoa kanuni ya kugawana madaraka kati ya wapinzani Salva Kiir na Riek Machar ndani ya serikali ya umoja wa kitaifa.

Lakini mvutano na ghasia vinaendelea katika nchi hiyo changa zaidi duniani, yenye utajiri wa mafuta lakini ambapo idadi kubwa ya watu wanaishi chini ya mstari wa umaskini. Baada ya kipindi cha mpito, uchaguzi ungelifanyika kufanywa Februari 2023. Lakini serikali hadi sasa haijaheshimu vifungu muhimu vya makubaliano kati ya Kiir na Machar, ikiwa ni pamoja na kuandaa Katiba.

Mwezi Agosti, viongozi hao wawili waliongeza muda wa serikali yao ya mpito kwa miaka miwili zaidi ya tarehe iliyopangwa, wakitaja matatizo katika kutekeleza makubaliano yao ya amani. Bw. Kiir, hata hivyo, aliahidi kuwa uchaguzi utafanyika mwaka wa 2024. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Nicholas Haysom, alionya mwezi Machi kwamba 2023 ulikuwa mwaka wa "kushindwa au kushinda" kwa Sudan Kusini, akitoa wito wa uchaguzi "jumuishi na wa kuaminika" mwaka 2024.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.