Hali ya demokrasia nchini Sudan inaendelea kuyumba
Nairobi – Dunia inaadimisha siku ya Demokrasia wakati huu hali demokrasia nchini Sudan ikiendelea kuyumba baada ya jeshi kumuondoa rais wa muda mrefu madarakani Omar al Bashir, mwaka 2019.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Matumaini ya wananchi wa Sudan, kuongozwa kidemokrasia, yameendelea kudidimia baada ya vita kuzuka kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF tangu Aprili 15.
Mpaka sasa jitihada za Kimataifa na kikanda kujaribu kurejesha hali ya kidemokrasia na kukomesha vita, hazijazaa matunda.
Hassan Khannenje ni mtafiti wa masuala ya kikanda kutoka Shirika la Horn, anathmini kinachoendelea nchini Sudan akiwa jijini Nairobi.
“Inaonekana kuwa wanaopigana Khartoum wana imani na wakuu wa nchi jirani ya Sudan Kusini, kutatua na kumaliza mapigano, Sudan ilisaidia kwa kiwango kikubwa katika mchakato wa kurejesha amani Sudan kusini, Ni dhahiri kuwa Sudan iko tayari kukaribisha Sudan kusini katika juhudi za kumaliza mapigano yanayoendelea. ” alisema Hassan Khannenje ni mtafiti wa masuala ya kikanda kutoka Shirika la Horn.
Hassan Khannenje ni mtafiti wa masuala ya kikanda kutoka Shirika la Horn
Mchambuzi wa siasa za Kimataifa na uhusiano wa Kimataifa Profesa Macharia Munene, anasema Sudan ina safari ndefu kupata demokrasia thabiti.
“Wakati uhuru umetoweka popote, kutoweka kwa uhuru huo unamaanisha utumwa. Una maana kuwa nchi haizwei kufikiriwa kuwa huru. Kwa njia nyingine kuwepo kwa demokrasia ni kuwa huru. Kukosekana kwa uhuru ni kutoweka kwa demokrasia. ” alieleza Mchambuzi wa siasa za Kimataifa na uhusiano wa Kimataifa Profesa Macharia Munene.
Mchambuzi wa siasa za Kimataifa na uhusiano wa Kimataifa Profesa Macharia Munene
Baada ya kuondolewa madarakani kwa Omar Hasan El Bashir, kulikuwa na jitihada zikiongozwa na Umoja wa Mataifa, ili kurejeshwa demokrasia mwaka 2023 lakini dalili zinaonesha kuwa itachukua muda mrefu.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Perthes Volker, ambaye amekuwa akiongoza jitihada hizo alitangaza kujiuzulu siku ya Jumatano.
Taarifa ya mwandishi wetu wa masuala ya Sudan James Shimanyula.