Pata taarifa kuu

Serikali Tanzania yakanusha kuwazuilia wakosoaji wa mkataba wa bandari

Nairobi – Serikali ya Tanzania, imekanusha madai kuwa watu watatu wanaoshikiliwa na idara ya polisi akiwemo balozi wa zamani wa taifa hilo nchini Canada, walikamatwa kwa sababu za kukosoa mkataba wa uwekezaji wa bandari kati ya Tanzania na Serikali ya Dubai.

Ramani ya nchi ya Tanzania
Ramani ya nchi ya Tanzania © https://wwwnc.cdc.gov/
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake waziri wa habari Nape Nnauye, amesema watatu hao,  Boniface Mwabukusi, Mpaluka Nyangali na Dkt Wilbroad Slaa, walikamatwa kwa kutoa matamshi ya uchochezi yenye kuhatarisha usalama ikiwemo njama ya mapinduzi.

Waziri Nnauye amesema, watuhumiwa hao walitoa wito hadharani kwa raia kuwashikia silaha polisi, na kukamatwa kwao ni onyo kwa wengine wenye mawazo kama hayo na wala si kuminya uhuru wa kujiuleza.

Aidha ameyakashifu mashirika ya ndani na yale ya kimataifa kwa kuchapisha habari ambazo amesema ni zapotoshaji kuhusu sababu hasa za raia hao kukamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.